- Isajili Biashara Yako
Katika hatua hii, unapaswa kuwa umefanya utafiti wa kina wa soko ili kuamua juu ya bidhaa au huduma unazokusudia kutoa pamoja na wateja wako walengwa. Baada ya hapo, hatua inayofuata ni kuisajili biashara hii ili upate leseni ya biashara online. Kwa kufanya hivyo, utaihalalisha biashara yako kisheria na hivyo kuongeza nafasi yako ya kupata ufadhili kutoka kwa wawekezaji binafsi au kupata mikopo kutoka kwa taasisi za fedha. Utahitaji pia kusajili jina la biashara. - Tambua Mbinu Mwafaka Mtandaoni
Kulingana na biashara ya online unayofanya, unaweza kuchagua kutumia soko la mtandaoni lililojengwa tayari (ecommerce platform), au kwa kujijengea tovuti yako mwenyewe, au utumie njia mseto. Masoko ya kimtandaoni ambayo unaweza kutumia kuuza biashara zako ni pamoja Jumia, Zudua, Kilimall, na mengine mengi. Hata hivyo, kwa kutumia majukwaa kama haya, itakugharimu ada fulani lakini Kwa Kinange App ni Bure.
Vilevile, unaweza kujijengea tovuti yako mwenyewe kupitia Shopify, WordPress, WooCommerce na BigCommerce. Mbinu hii itakuwezesha kudhibiti jinsi unavyotaka mwonekano wa tovuti yako uwe. Ni muhimu kutathmini kwanza jinsi tovuti mbalimbali zilivyo kabla ya kufanya uchaguzi dhahiri. Ili kupanua idadi yako ya wateja, unaweza pia kutumia mbinu mesto; ambayo inahusu kutumia soko la mtandaoni na pia tovuti yako binafsi.
- Amua Kuhusu Mkondo wa Malipo Unaokufaa
Unaweza kuchagua kupeana akaunti ya benki kwa wateja kuwekea amana ya malipo au kutumia njia hizi za mtandao za malipo kwa ajili ya biashara barani Afrika. Kwa kutegemea nchi ya Afrika unamohudumia, njia hizi za mtandao za malipo zinajumuisha malipo kwa pesa rununu, PayPal, n.k. Kama utakuwa unahitaji teknolojia ya kupokea malipo kwa njia ya kadi (debit card na credit card) basi utahitaji kutumia huduma za malipo mtandaoni kama vile MFS Africa, Flutterwave, PesaPal miongoni mwa nyingine.
Hapa Kinange tunatumia njia rahisi Kwa mteja kufanya malipo ambayo ni nyia za lipa number, mpesa, bank nk.
- Anza kuuza
Usisubiri hadi kila kitu eti kionekana kuwa kamilifu. Kama ilivyo kwa maduka halisi, biashara ya mtandaoni huchukua muda wa kufikia kiwango unachokitaka. Ili kufanikisha mauzo, unaweza kutumia mitandao ya kijamii, maonyesho, punguzo (discount), matukio muhimu, na hata mapendekezo kutoka kwa wateja wa awali. Uwezeshaji wa Kusaka Mtandaoni (Search Engine Optimisation) pia ni njia unayoweza kutummia ili kuwavutia watu zaidi kwenye tovuti au duka lako la mtandaoni. Tumia pia Google ili kupata miongozo mbalimbali ya jinsi ya kupata wateja mtandaoni au jinsi ya kutangaza biashara mtandaoni. - Uwasilishaji wa Bidhaa Unaoaminika
Kulingana na nchi unamoendeshea biashara, unaweza kutumia usafiri wa umma unaoaminika ili kufikisha bidhaa zilizonunuliwa. Pia, unaweza kuwasiliana na kampuni za kutuma mizigo na bidhaa kama vile Posta au kampuni chipukizi za usafirishaji haraka wa mizigo au huduma nyingineyo ili kuwafikia wateja wako.
Hitimisho la Biashara Mtandaoni
Sawa na mabara mengineyo, Afrika inapitia maendeleo makubwa ya kiteknolojia. Biashara ya mtandaoni ni mojawapo ya maendeleo hayo. Ukianzisha duka la mtandao na ukiwa unajua jinsi ya kuuza bidhaa mtandaoni au kutoa huduma mtandaoni, utapata fursa ya kuwafikia wateja wengi sana na kupata faida kubwa. Ikiwa utafuata hatua zilizojadiliwa katika makala haya, kama mwekezaji utakuwa umejihakikishia mafanikio ya biashara za online.