Biashara ya mtandao ni namna moja ya kufanya biashara inayokua kwa kasi kubwa zaidi katika karne tuliyo nayo sasa.

Sisi kama Kinange company tumeamua kuanzisha kampuni hii Kwa lengo la kuwasaidia wafanya biashara wengi kuuza bidhaa Nchi nzima. Ni kweli ukiwa na duka Arusha huwezi uzia watu wa njombe au Geit lakini kupitia mtandao wateja wataweza kuona bidhaa zako na kuplace orders.

BIASHARA ZA MTANDAONI
Wakati hazihitaji mtu kuwa na cheti cha masomo, zinahitaji mfanyaji kuwa na tabia tofauti kidogo na ya mtu aliyezoea kuajiriwa. Hizi ni biashara ambazo mtu anayeshiriki atakuwa mwamuzi wa kila jambo linalohusu biashara yake, akishaanza kufanya biashara hii hakutakuwepo na mtu wa kumsukuma na kumsimamia. Yeye huwa ndiye bosi wa biashara yake

ANZA SASA KUUZA NA KINANGE
Unaweza kuanza biashara ya mtandao kwa mtaji mdogo sana au kwenye kampuni nyingine bila kuwa na mtaji kabisa. Hakuna tofauti kati ya yule aliyeanza na mtaji mdogo na yule aliyeanza na mtaji mkubwa, fursa zenu za kufika mnakotaka zinafanana na kubwa kuliko fursa utakayopata kwenye mifumo mingine ya biashara.

Pamoja na kuwa pengine utaanza biashara yako bila mtaji wo wote, utahitaji kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako ikiwa ni pamoja na kununua bidhaa, mawasiliano, usafiri, matangazo n.k.

Sisi Kinange ni kampuni kwahiyo kama mfanyabiashara huhutaji kulipa ada zozote Ili kujiunga.

UTENDAJI KAZI
App ya Kinange ni kama apps nyingine za biashara mtandaoni kubwa duniani kama Amazon, Alibaba nk, mfanyabiashara utaweza kuwa na akaunti Yako na kupakia bidhaa ndani ya dakika 1.

Wateja ulimwengu kote ikiwemo Tanzania wataweza kuona bidhaa zako na kuweka order. Huhutaji elimu Wala ujuzi wa kompyuta Ili uweze kuanza biashara hii.

MAFUNZO
Biashara za mtandao hazihitaji uwe na uzoefu wa kuuza, wala hazihitaji uwe umepata mafunzo ya biashara. Kuwa na uzoefu huo au mafunzo hayo ni kitu kitakachokusaidia, lakini kila mwanachama anayejiunga na biashara hizi hupewa mafunzo ya kutosha. Mafunzo hayo utayapata kutoka kwenye kampuni au kutoka kwa mtu wa juu yako (aliyekusajili). Kampuni nyingine hutoa mafunzo ya aina mbali mbali kwa wanachama wao, hutoa mafunzo darasani, CD, DVD, vipeperushi, vijitabu vya kujisomea na hata kwa njia ya mtandao (internet).

MAHITAJI
Kunaza biashara hii ya mtandao unahitaji kuwa na smartphone pia bundle Ili uweze ku upload bidhaa zako.

Bidhaa(ni picha za bidhaa husika mfano picha za simu ilivyo na sifa zake) pia mfanyabiashara atajipangia Bei ya kuuza bidhaa zake.
Mfanyabiashara ataweza kuweka punguzo Kwa wateja wake, kupata SMS za orders pale wateja watakapo order bidhaa zake hata kama hayupo online.

Mfanyabiashara ataweza kuandika sifa za bidhaa zake Kwa kifupi mfano, ni nyeusi na nyepesi nk.
Pia, ataweza kuona orders Kwa dashboard yake na malipo mfanyabiashara atapokea kabla ya kutoa/kutuma bidhaa

KUFANYA BIASHARA POPOTE
Maendeleo ya teknolojia yanamwezesha mfanya biashara ya mtandao kufanya shughuli zake po pote alipo. Ukiwa na simu ya kiganjani unaweza kuwasiliana na wateja wako kutoka po pote ulipo.

Ukiwa umeunganishwa kwenye internet, unaweza kuchukua simu yako au lap top yako na ukaendelea kufanya biashara zako ukiwa safarini, ukiwa kwenye mapumziko, ukiwa umekwenda kuwaona ndugu walio kwenye mji mwingine na hata ukiwa nchi nyingine.